Jumamosi kanda ya Dar Es Salaam na Pwani walikuwa na tukio lao maalumu la kuwaona wagonjwa hospital ya Ocean Road Dar Es Salaam .
Tukio hili lilihudhuriwa na wana sadaka wa kanda hii takribani watu 60 .Kutokana na mazingira na taratibu za hospital, hawakuhitaji kununua mahitaji yoyote kwenda nayo badala yake wana kanda walichanga sadaka zao na kufikisha kiasi cha TZS 1,000,000/= (Milioni Moja ) ambacho walienda nacho hospital !
Uongozi wa hospital ulitupatia control namba za wagonjwa 20 ambao kupitia kiasi cha TZS 1M tuliweza kusaidia malipo kidogo ya matibabu kwa kila mgonjwa ,wastani wa TZS 50,000/= kila mgonjwa alilipiwa kwenye akaunt yake ya Bill ya hospital !
Wana Sadaka wa kanda wanaushukuru Uongozi wa Sadaka Yetu ,wanasadaka wote kwa maombi na kibali katika kufaninikisha zoezi hili la jana.
Pia uongozi wa Hospital wa Ocean unatushuruku sanaa kwa majitoleo yetu ya kusaidia wahitaji ,na kwa watu mbalimbali waliokuwa hospital walishawishika kwa huduma hii na kutupatia namba zao kujiunga nasi moja kwa moja !
Mungu atubariki sote !
#SADAKA YETU KWA AJILI YA WENGINE!