Skip to content

CHANGIA

Kila mchango wako, mkubwa au mdogo, unabadilisha maisha ya mgonjwa anayesubiri faraja, familia inayohitaji msaada wa haraka, au mtu anayepitia wakati mgumu. Jiunge nasi kufanya upendo uwe wa vitendo.

 KWA NINI UCHANGIE?

Mchango wako unatusaidia:

  1. Kuwatembelea Wagonjwa
    Kuwafikia wagonjwa mahospitalini kama Ocean Road Cancer Institute kwa faraja na uwepo wa kweli.
  2. Kupeleka Mahitaji
    Kununua na kupeleka chakula, vifaa, na mahitaji muhimu kwa walio katika hospitali au majumbani.
  3. Kusaidia Bili za Matibabu
    Kuchangia gharama za matibabu kwa wagonjwa walioshindwa kulipa wenyewe.
  4. Kusimama na Familia za Msiba
    Kutoa faraja na msaada wa moja kwa moja kwa familia zinazopitia msiba.