Wanasadaka Washiriki Kuchangia Damu na Kuwafariji Watoto Waliolazwa Mount Meru

Picha ya pamoja ya Wanasadaka walioshiriki katika zoezi la kuchangia damu na kutembelea watoto waliolazwa katika Wodi ya Watoto ya Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru, Arusha.

Tukio hili liliandaliwa na Taasisi ya Sadaka Yetu kwa lengo la kuhamasisha uchangiaji wa damu, kuwafariji watoto waliolazwa hospitalini na kukabidhi mahitaji muhimu.

Tunawashukuru Wanasadaka wote kwa moyo wa upendo, mshikamano na kujitoa kwa ajili ya kuwahudumia wengine. Mungu awabariki kwa wingi. ❤️🩸🙏

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Scroll to Top